Tuesday, September 13, 2011

SAIDIA NDUGU ZETU WA ZANZIBAR….

Baada ya Ijumaa ya tarehe 10 September 2011,meli ya M.V. Spice Islander,inayofanya safari kati ya Dar es Salaam,Zanzibar,Pemba na Tanga,ilizama baharini ikielekea Pemba na ilikua na abiria zaidi ya 610na zaidi ya 200 kufariki na wengine 500 kuokolewa wakiwa hai
Imeanzishwa taasisi ya Saidia Zanzibar www.saidiazanzibar.org na ni emergency fundraising website,yenye lengo la kuwahamasisha wasamaria wema popote walipo,kuchangia kwa hali na mali wahanga na familia zilizopatwa na janga hili na taasisi hii itasimamiwa na Zanzibar Association of Tourism Investors www.zati.org,registered NGO,ambayo itaratibu michango kupitia ofisi yao iliyopo Cine Afrique Malindi,Stone Town- Zanzib
Kwa maelezo zaidi watembelee kwa maelezo zaidi saidia@saidiazanzibar.org

MWISHO AFANYA KWELI KWA MERYL MJUMZITO …


 Baada ya kuvalishana pete za uchumba kwenye jumbla la Big Brother Africa, kwa sasa kuna rumours kuwa aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Africa,Meryl Shikwambane toka Namibia kwa sasa ni mjamzito na Mwisho Mampamba ndiye 'baba mtarajiwa'
ENGAGEMENT PARTY NDANI YA BBA HOUSE....SEPT 25,2010
Mwisho na Meryl watakua wamefuata nyayo za washiriki wengine wa Big Brother Africa,Quinn na Jennifer ambao wanategemea kupata mtoto karibuni,Kevin na Liz ambao walioana mwaka jana na kubarikiwa mtoto wao wa kwanza Malaika

MOVIE ZA HIP HOP ZAPATA SHAVU MAREKANI

Movie zenye mahadhi ya Hip-Hop zimepata shavu kwenye tamasha la 15 za Annual Urban World Film Festival,pande za New York City-Marekani
THINGS FALL APART - MOVIE
Movie ya 50 Cent,Things Fall Apart,Planet Rock:The story of Hip-Hop and The Crack Generation,I Want My Name Back na movie yenye utata ya Outside In: The Story of Art in the Streets zitaoneshwa kwenye tamasha hilo la siku 5 na tamasha hilo linatarajiwa kuanza September 14 mpaka 18,2011 pande za AMC Theater,34th Street – Midtown,Manhattan na filamu 59 zinatarajiwa kuoneshwa
PLANET ROCK - MOVIE

JUSTIN BIEBER ATANGAZA NDOA

JUSTIN DREW BIEBER
Justine Bieber amefunguka kuwa anataka kufunga ndoa na kuwa na watoto katika kipindi cha miaka 10 ijayo.Kwa sasa BiebStar ana miaka 17 na akiwa na miaka 25 au 26, anataka awe na familia na kudai kuwa anataka afanye mambo yake kwenye kipindi hicho cha ujana coz anataka awe baba kijana mwenye familia na uhuru wa kufanya vitu atakavyo kama movie nk,Lakini hajafunguka kama atamuoa demu wake Selena Gomez au vp....
JUSTIN BIEBER NA GAL-FRIEND WAKE,SELENA GOMEZ

2PAC SHAKUR ATIMIZA MIAKA 15 YA KIFO CHAKE

TUPAC AMARU SHAKUR (JUNE 16,1971 - SEPT 7,1996)
Leo imetimia miaka 15 ya kifo cha Rapper,Tupac Amaru Shakur aka 2 Pac au Makaveli aliyezaliwa June 16,1971 na kupigwa risasi September 7,1996 na kufariki dunia September 13,1996 2 Pac amepewa heshima kama the father's of West Coast hip-hop,na kumfanya awe the most successful deceased rapper in the game,Na kwa kuthamini na kutambua mchango wake kwenye game,mji wa Herford ulioko nchini Ujerumani uliweka sanamu la 2 Pac Shakur kwenye makumbusho yake ya Marta....
MARTA MUSEUM - HERFORD,GERMANY
Mama yake,Afeni Shakur alianzisha Shakur Family Foundation na baadaye kuiita Tupac Amaru Shakur Foundation au TASF mwaka 1997 iliyokua na lengo la kutoa training na support kwa wanafunzi wenye talents na hit song yake ya Dear Mama, ilikua ni moja ya nyimbo 25 zilizoingizwa kwenye National Recording Registry mwaka 2010 na kutajwa Dear Mama ina ujumbe kwa mama wote wanaokabiliwa na changamoyto maishani lakini wanazitunza familia zao na jamii kwa ujumla

AFENI SHAKUR DAVIS - 2 PAC SHAKUR'S DEAR MAMA

WATANZANIA WOTE TUUNGANE KUOMBOLEZA, MAAFA MAKUBWA YALIYOTUPATA




TUKO PAMOJA NA WATANZANIA WENZETU WALIOPOTEZA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KWA KUOMBOLEZA MSIBA HUU MKUBWA WA TAIFA ULIOTOKEA VISIWANI ZANZIBAR,TUSAMEHEANE BUT NADHANI KAMA ITAKUA POA SANA TUKIKUTANA TENA KESHO KWENYE MATIN'GA MENGINE MUNGU AKIPENDA....