Monday, July 04, 2011

Master advanced features - Share

Master advanced features - Share

THE MAKING OF KAMA IPO BY PROF JAY

Takribani mwezi mmoja uliopita, Professor Jay(The HeavyWeight MC) aliachia wimbo wake wa kwanza kutoka katika album yake mpya inayotarajiwa kuingia kitaani baadae mwaka huu.Baada ya hapo,na kama ilivyo ada,kilichokuwa kinafuata ni kutengeneza video ya wimbo huo ambao mpaka hivi sasa wapenzi wengi wa muziki wametokea kuupenda na kuukubali(kwanini usiupende?). You heard it,now you’ll have to see it!
Video hiyo ambayo inatarajiwa kutoka ndani ya wiki hizi mbili,inatengenezwa na Visual Lab chini ya usimamizi wa Adam Juma(naomba nimuite Mzee wa Next Level).Kama ulivyo wimbo wenyewe,video inatarajiwa kuweka bayana jinsi gani maisha yanaweza kupanda na kushuka.Ukiwa huna hivi leo,usikate tamaa.Fanya kazi kwa bidii kwani kesho yaweza kuwa zamu yako ya kupanda.Na kama leo unazo,basi nenda taratibu ili hata utakaposhuka,isiwe kinoma noma.