Tuesday, August 23, 2011

HATIMAYE BABA YAKE OBI MIKEL AOKOLEWA NA POLISI NIGERIA

MZEE MICHAEL OBI
Polisi wa Nigeria wamesaidia kumuokoa baba wa mwanasoka wa Chelsea na timu ya taifa ya Nigeria John Mikel Obi
Wateka nyara walikua wanadai mkwanja Naira milioni 20 za Nigeria ili wamuachie Mzee huyo na Maofisa wa Polisi walivamia pande za mji mmoja ulio nchini Nigeria wa Kano na kumkuta Mzee Michael Obi na kuwakamata washukiwa 5 na wanaodaiwa kuhusika na utekaji nyara huo,wakati Mzee Obi akitoka kazini kwenye mji wa Jos kuelekea home kwake tarehe12 August,2011 na Mzee Obi alifunguka kuwa walimpa kichapo cha kiaina.... cha kishkaji...!

JOHN MIKEL OBI (CHELSEA & NIGERIA)