Wednesday, July 11, 2012

MJADALA MKALI KATI YA LIONEL MESSI NA RONALDINHO GAUCHO MKALI NANI?- VALDES WA BARCA KAMCHAGUA RONALDINHO




Kipa wa Barcelona Victor Valdes amesema amecheza na wachezaji wote wawili Ronaldinho na Lionel Messi lakini kwa asilimia 100 anaamini Gaucho alikuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa kuliko wote ambao amewahi kuwashuhudia akiwemo Messi. Kipa huyo mwenye miaka 30, aliiambia Terra TV. Akiwa anatajwa sana kama mmoja ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea ulimwenguni, Messi ameuwasha moto kwenye La Liga katika kipindi cha miaka 8, akivunja rekodi mbalimbali ikiwemo ya kufunga mabao mengi. Lakini, Valdes anaamini Ronaldinho kipekee zaidi aliibadilisha historia ya Barca alipowasili Nou Camp 2003, na kuchangia kwa mafanikio wanayoyapata kikosi cha sasa. "Siku zote nimekuwa nikisema kwamba Rony aliibadilisha historia ya klabu alipokuwa akicheza hapa. Alikuwa kiongozi wa timu ambayo ilibadilisha histori yetu. "Hatukuwa tumeshinda taji lolote kwa miaka mingi. Alikuja na kuifanya Barca kuwa na nguvu na kuifanya kuwa klabu kubwa inayojulikana duniani kote kwa uwezo wake. Namshukuru sana kwa hilo. Naweza kusema ndio mchezaji mwenye kipaji kikubwa kuliko wote ambaye nimewahi kushea nae chumba cha kubadilishia nguo. Alikuwa anafanya vitu vyake vya kustajaabisha kila siku. 

No comments: