Saturday, June 18, 2011

Video: Chris Brown f/ Justin Bieber – ‘Next 2 You’

Chris Brown ameachia video yake mpya ya ngoma ambayo ipo kwenye Album yake mpya inayoitwa F.A.M.E...R&B superstar huyu ameunganisha nguvu zake yeye na Justin beiber dogo ambae kwasasa level yake katika music haishkiki....katika video hii madogo wanaonekana kama ni watu waliokua wakipendana sana na wapenzi wao na kisha ghafla yanatokea maafa makubwa ambayo yanawasababisha kupoteana na wapenzi wao hao ndipo hapo Chris Brown anaonekana akiwa anamtafuta demu wake kila kona na hatimae mwisho anakuja kumkuta demu wake huo amegongwa na gari huku Justin Beiber akiwa amefanikiwa kukutana na mpenzi wake nakuonesha ulimwengu kwamba sasa amekua yani kisha kula kile kitu cha kiss live kwenye video.....

New Music: 50 Cent – ‘Outlaw’

50 Cents amerudi tena kwenye speakers zako na kitu cha "Outlaw" hii ni ngoma yake mpya ambayo ndo inatambusha Album yake ya tano ambayo anategemea kuitoa hivi karibuni....kwenye nyimbo hii mtu mzima kama kawaida yake amediss watu kibao yani ukisikiliza vizuri utajua kabisa watu ambao amewadiss japokua hajawataja majina yao ni bonge la ngoma yani huu ndio ujio wa 50cents watu waliokua wanasubiria sikiliza track hii alafu tupia comment yako unazungumziaje kuhusu ujio huu mpya wa Curtis Jackson a.k.a 50cents.......