Tuesday, May 22, 2012

MOURINHO ASAINI MKATABA MPYA WA KUBAKI MADRID MPAKA 2016


Jose Mourinho amewakata maini Chelsea na Roman Abramovicha baada ya kusaini mkataba mpya  na Real Madrid utakaoenda mpaka 2016.
The Special One, ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kurudi Chelsea  alisaini mkataba wa miaka minne in May 2010. Lakini kocha huyo raia wa Ureno amekubaliana vipengele vipya katika dili hii mpya ya miaka miwili.
Mourinho ameiongoza kushinda Copa del Rey katika msimu wake wa kwanza pale Bernebau na hivi karibuni ameleta kikombe cha ubingwa wa La liga ambacho kilikuwa kimepotea machoni mwa Madrid kwa muda mrefu kidogo.

DIDIER DROGBA ATHIBITISHA KUONDOKA CHELSEA


Siku mbili baada ya kuiwezesha klabu yake ya Chelsea kushinda kombe la mabingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza, mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba leo hii amewaambia wachezaji wenzie kwamba anaondoka Chelsea.

Shujaa huyo wa Champions league amekiri kwamba hayupo tayari kukaa benchi.
Akiwa na hisia kali Drogba, 34, alionekana kulia alipokuwa akiwaambia wachezaji wenzie wa Chelsea uamuzi wake wakati wakiwa msafara wa kusherehekea ubingwa mitaani jana.

Didier ambaye mkataba wake unaisha mwezi ujao pale Stamford Bridge, ameliambia jarida la France Football: "Hatutakuwa pamoja msimu ujao. Nilipoamua kuwaambia, nilitaka niwaambie hivyo, lakini walinifanya nipotezee ujasiri. Hata hivyo ni miaka mitatu sasa imepita tangu niseme nataka kuondoka - napata wakati mgumu sana kukiri kwamba nimefikia mwisho kuwa hapa, lakini siwezi kukubaliana na ukweli wa kukaa benchi na kuangalia wachezaji wengine wakicheza wakati klabu itakapoamua kuja na mipango ya kutengeneza timu upya."

Drogba ambaye amekuwa akihusishwa na kwenda kuungana na Anelka huko katika klabu ya Shanghai Shenhua aliongeza: "Hivyo ndivyo ilivyo - najiandaa kwenda sehemu nyingine ambayo sijaijua bado. Itakuwa kitu kingine tofauti."

KUINUNUA MAN UNITED INABIDI UJIPANGE : PAMOJA NA KUKOSA KOMBE LOLOTE MSIMU HUU – YATAJWA KAMA TIMU YENYE THAMANI KUBWA KULIKO ZOTE


THE BRAND FINANCE FOOTBALL TOP 25 FOR 2012

2012 RANK
2011 RANK
CLUB
LEAGUE
BRAND VALUE
CHANGE IN VALUE
1
1
Man Utd
England
€672.9m
29 %
2
4
Bayern
Germany
€617.9m
59 %
3
2
Real Madrid
Spain
€471.7m
-7 %
4
3
Barcelona
Spain
€455.9m
-8 %
5
5
Chelsea
England
€312.9m
27 %
6
6
Arsenal
England
€305m
29 %
7
9
Liverpool
England
€288.5m
47 %
8
11
Man City
England
€237.4m
77 %
9
7
Milan
Italy
€229.5m
7 %
10
12
Schalke
Germany
€209.1m
97 %
11
15
 Dortmund
Germany 
 €178.4m
 81 %
12
 14
 Tottenham
England
 €176.8m
 77 %
13
 8
 Inter
Italy 
€169m
-18 %
14
 23
 Ajax
 Netherlands
€144.6m
 150 %
15
 17
 Marseille
 France
 €132.1m
 41 %
16
10
 Juventus
Italy
€125.8m
 -13 %
17
 13
 Hamburg
Germany 
€120.3m
14 %
18
 16
 Lyon
 France
 €94.3m
 -1 %
19
 25
Aston Villa
England  
 €68.4m
27 %
20
 NEW
 Newcastle
England  
 €67.6m
115 %
21
 18
 Roma
Italy 
 €66.8m
-16 %
22
 24
 Napoli
Italy 
 €66.8m
 22 %
23
 27
 Everton
England 
 €62.1m
 28 %
24
 NEW
 Corinthians
 Brazil
 €60.5m
 NEW
25
 22
 Bordeaux
 France
€59.7m
-2 %