Tuesday, May 22, 2012

DIDIER DROGBA ATHIBITISHA KUONDOKA CHELSEA


Siku mbili baada ya kuiwezesha klabu yake ya Chelsea kushinda kombe la mabingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza, mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba leo hii amewaambia wachezaji wenzie kwamba anaondoka Chelsea.

Shujaa huyo wa Champions league amekiri kwamba hayupo tayari kukaa benchi.
Akiwa na hisia kali Drogba, 34, alionekana kulia alipokuwa akiwaambia wachezaji wenzie wa Chelsea uamuzi wake wakati wakiwa msafara wa kusherehekea ubingwa mitaani jana.

Didier ambaye mkataba wake unaisha mwezi ujao pale Stamford Bridge, ameliambia jarida la France Football: "Hatutakuwa pamoja msimu ujao. Nilipoamua kuwaambia, nilitaka niwaambie hivyo, lakini walinifanya nipotezee ujasiri. Hata hivyo ni miaka mitatu sasa imepita tangu niseme nataka kuondoka - napata wakati mgumu sana kukiri kwamba nimefikia mwisho kuwa hapa, lakini siwezi kukubaliana na ukweli wa kukaa benchi na kuangalia wachezaji wengine wakicheza wakati klabu itakapoamua kuja na mipango ya kutengeneza timu upya."

Drogba ambaye amekuwa akihusishwa na kwenda kuungana na Anelka huko katika klabu ya Shanghai Shenhua aliongeza: "Hivyo ndivyo ilivyo - najiandaa kwenda sehemu nyingine ambayo sijaijua bado. Itakuwa kitu kingine tofauti."

No comments: