Thursday, September 08, 2011

KANYE WEST APIGA SHOW NA D’BANJ LONDON !


Rapper Kanye West alifanya surprise appearance kwenye Mo'Hits Koko Concert ambayo artist wake D'Banj alikua anapiga show iliyofanyika jijini London nchini Uingereza
D'banj,ambaye amepata shavu kwenye label ya Kanye West ya G.O.O.D Music,alifanya surprise introduction on stage,na Kanye kupiga ngoma yake ya All Of The Lights na kufanya fans waliokuja kwenye concert hiyo wapagawe mbayaaa na baadaye D'banj na Producer wake Don Jazzy walifunguka kwenye mtandao wa Tweeter kwa kumshuku Kanye West kwa support.....

MOWZEY RADIO APIGA DEM MPAKA ALAZWA !


MOSES SEKIBOOGO NAKINTIFE – MOWZEY RADIO
GoodLife Crew toka Uganda wameendeleza series za ku-make headline kwenye music industry ya Uganda baada ya kumpa vitasa kadhaa shosti mmoja aliyeleta za kuleta
GOODLIFE CREW
Issue imetokea pande za Casablanca wakati mdaa toka Sudan aliyetumwa kuwapelea 'kanywaji' aina ya Black Label kwenye meza yao kuanza ku-talk sh*t kwa Mowzey Radio kuwa kwa sasa GoodLife wamefulia mbaya nawanaendesha magari ya bei chee na ndipo kipondo kama mvua toka kwa Radio kilipoanza na kumsababisha dada huyo kwa sasa kuwa kwenye coma,japo mabausa nwa club hiyo kumuokoa kwa kumtoa Mowzey Radio nje ya club....

CURTIS JAMES JACKSON III - 50 CENT
Bosi wa G-Unit,Curtis James Jackson III aka Rapper 50 Cent amezindua mpango wake kwenye Twitter uitwao SK Initiative na kuingia ubia na kampuni toka New York ya Pure Growth Partners mwezi uliopita na ku-release kinywaji cha the Street King Energy shot natural juice,na mauzo yake kusaidia watoto wapatao bilioni 1 barani Africa wanaokabiliwa na njaa....

 STREET KING ENERGY DRINK (SK MOVEMENT)
Kwenye project video ya ya SK movement,50 Cent amefunguka umuhimu wa dunia kupinga njaa na kuongeza kuwa amezaliwa bila mkwanja,lakini hajawahi kulala na njaa na kuna watu wengi wanakufa kwa njaa na ni jukumu letu kuungana pamoja kutafuta suluhisho la tatizo hilo

KIDUM,REDSAN NA HABID WATOA VIDEOZ MPYA

HABIDA MALOONEY - KENYAN ARTIST 
Beautiful singer Habida toka Kenya,ame release video yake mpya iitwayo My Reason featuring Canibal toka Momba.Video imegongwa na Producer Robert Kamanzi aka R-Kay,na location ya video hiyo imefanyika jijini Mombasa kwenye beach kali na directer Emmanuel Jambo amehusika
SWABRI MOHAMED AKA REDSAN - KENYAN DANCEHALL ARTIST
King of dancehall wa East Africa,Swabri Mohammed aka Redsan toka Kenya amedondosha kichupa cha Brand new video yake inayokwenda kwa jina la Ila Wewe ambayo iko kwenye album yake ya versatility,na humu ndani ameonesha kipaji cha kuimba zaidi ya dancehall skills alizonazo
JEAN PIERRE NIMBONA AKA KIDUM - BURUNDI/KENYAN MUSICIAN
Msanii bora wa mwaka wa Tuzo za East Africa Music Awards-2011, Jean Pierre Nimbona aka Kidum naye ameachia video ya ngoma yake iliyopata sana airtime,Mulika Mwizi featuring Sanaipei Tande aka Sana ambayo ni single ya kwanza ya kwenye album yake ya 5.Producer Robert Kamanzi aka R-Kay amehusika na production nzima ya video hiyo kali