Kibao chake cha pili kutoka kiliitwa 'Binti Malkia' ambacho alimshirikisha Noorelly. Ilivyofika mnamo mwaka wa 2004 Fid Q alivunja ukimya wake kwa kibao chake mahili kilichokwenda kwa jina la "Fid Q.com", na kibao hicho alikifanya katika studi ya Baucha Records baada ya kuhama kwa MJ.
Kibao hicho kiliirudisha ile hiphop ya Tanzania katika ramani yake halisi na inasemekana hivyo kwasababu kipindi hicho ni kile ambacho wasaanii wengi wa muziki wa kufokafoka walikuwa wamejiingiza katika masuala ya uimbaji kwasababu kulikuwa na uvumi wa kwamba hip hop haikubaliki kwa watu wa Tanzania.
Ilipofika mwezi wa Januri ya 26 katika mwaka wa 2008, Fid Q alipakua kibao kiitwacho "Ni Hayo Tu" alichomshirikisha Prof. J na Langa. Kibao hicho kilibahatika kujinyakulia Tuzo ya Kili kikiwa kama kibao bora cha muziki wa hip hop kwa mwaka wa 2007-2008.
Fid Q ana albamu mbili kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa inayoitwa "Vina Mwanzo Kati na Mwisho".[1] Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili "PROPAGANDA", ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic'. Hivi karibuni anategemea kutoa albamu yake ya tatu itakayokwenda kwa jina la "KitaaOLOJIA".