Sunday, March 10, 2013

Saturday, March 02, 2013

Thursday, September 06, 2012

Z-Anto’’SIKUJUWA KAMA ‘JAFFARAI’NI KAKA YANGU MIAKA YOTE!!

MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Z-anto, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa hakuna kitu alichokuwa anakijua kuhusiana na msanii mwezake Jaffarai, lakini msiba uliotokea nyumbani kwao Mtwara ndiyo uliowakutanisha na hadi wao kujuana kuwa wao ni ndugu wa damu , ambapo Jaffarai ni kaka yake. Msanii huyo aliichambua story nzima hadi alipojua ishu hiyo kuwa Jaffarai ni kaka yake, kuwa kuna siku moja alienda kusalimia nyumbani kwa Mtwara na alipofika huko, aliambiwa kuwa Jaffarai katoka hapo kwao muda si mrefu, na baada ya hapo alijiulizia maswali mengi kwamba jamaa alienda kwao kufanya nini. Aliendelea kusema kuwa hakuendelea kuhoji na baada ya siku mbili ulitokea msiba hukohuko kwao, na alipoenda kule alianza kutambulishwa na mama yake kuwa Jaffarai ni kaka yake na hapo kwenye msiba kulikuwa na dada zake jamaa ambao nao ni dada zake huku mama yake akimwambia walishindwa kuwaambia kwani ni makosa ambayo tayari yalikwisha tokea. “Utambulisho ule ulinifanya niishiwe nguvu kwa sababu jamaa nilikuwa nashinda naye sana sehemu sehemu na hata yeye hakuwahi kunaimbia ishu hii nahisi alikuwa hajui, lakini hata hivyo nashukuru kwani sasa nimejua mshkaji ni kaka yangu na nafurai sana,” alisema Z-Anto. Hata hivyo alisema kuwa mama yake na mama yake Jaffarai wanaitana dada hivyo udugu wao si wa kufosi kwani kila kitu kilijulikana katika msiba huo uliowakutanisha na dada zake Jaffarai pamoja watu wengine ambao hakudhania kama waweza kuwa ndugu zake. TE!!