Friday, June 10, 2011

RAISI WA WASAFI” AFIKISHWA POLISI KWA MADAI YA SH. MILIONI 70…!!

MSANII wa Bongo Flava, Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz aka Rais wa Wasafi hivi karibuni kafikishwa polisi kwa madai ya kushindwa kurudisha mkwanja aliokopa! Diamond alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam akidaiwa kujipatia mamilioni ya mkwanja za jamaa aitwaye Msafiri Peter aka Papaa Misifa,ambapo ilidaiwa kuwa Diamond alimuomba ampatie milioni 30 ili atoe albamu yake na wakaandikishiana mkataba kuwa atakuwa akimpa asilimia flani kiaina ya mauzo na mapato ya shoo atazokuwa anafanya.

Lakini Diamond amekuwa akienda kinyume mkataba huo na kwa sasa anadaiwa shilingi milioni 70, yaani milioni 30 alizochukua na milioni 40 za fidia ya kuvunja mkataba huo…. Papaa Misifa amefunguka kukiri kumfikisha msanii huyo polisi na kumfungulia jalada la kesi lenye namba OB/RB/9343/11

Hivi sasa Diamond yuko nchini Sweden kupiga showz kadhaa

Ja Rule kaanza kifungo chake cha mwaka mmoja na nusu.

Ja Rule kaanza kifungo chake cha kosa la kukamwatwa na siraha kinyume cha sheria siku ya jana, Jamaa atakuwa jela kwa mda wa miezi 18 hadi 20, kitu cha kama mwaka mmoja na nusu hiviiiiii. Ndani ya huo mwaka mmoja na nusu ataachia album zake mbili mpya ambazo kamaliza kuzifanya juzi siku moja kabla ya kwenda jela.

Wakati anatoka mahakamani siku ya jana huku kafungwa pingu, tayari kwa safari ya kwenda jela, ndugu na marafiki zake waliojitokeza k**-support walilia sana pale alipo waaga akiwaambia kuwa “Tutaonana”…

Ndani ya Teentz.com unaweza kumuona Ja Rule live akiwa studio siku ya juzi akimalizia album zake na akijipa moyo huku akijilahumu kwa kuwa mtu

maarafu na akielezea swagga ambalo atakuwa analitumia akiwa jela ili watu wasije kumfanyia kitu mbaya ...dan ya jool new blog