Friday, September 16, 2011

ALIBUM YA BEBE COOL KUINGIA SOKONI OCTOBER…!

 
MOSES BIDANDI SSALI - BEBE COOL
Mwaka jana,Multi-talented Reggae,Ragga,Dancehall na Afro beat singer,Moses Ssali aka Bebe Cool alipiga show ya kutakata kwenye concert Big Size pande za Kati Kati Restaurant na kupata tuzo ya Pam awards artist of the year
Mwaka 2008 na 2009 Bebe Cool ali-launch tarehe sawa na hasimu wake Bobi Wine,lakini mwaka huu Bebe Cool ameamua kufanya uzinduzi wa album yake mpya ya Minzani,Ijumaa ya October 7,2011 'kishua zaidi' na atapiga show pande za Garden City Roof Top na kuendelea na showz 3 nyingine October 8 pande za Satelite beach Mukono,na October 9 pande za Maria Flo,Masaka
Bebe Cool ameshaachia hits songs Minzani,Sanyu Lya Mutima Gwange,Tumekuja Ku Party featuring Fidempa,Ceaze and Seakle featuring Rema,Dogo Lyo Featuring Tuff B kwenye concert zake hizo atapigwa tough na artist toka Gagamel kama Tuff B,Tickie Tah,Mr Woods na wengine kiba

LIL WAYNE ATOA DISS KWA JAY -Z

JIGGA vs WEEZY
Lil Wayne ametoa ngoma na Drake na Jadakiss inayoitwa,It's Good inayosemekana ni diss-Track kwa Rapper Jay Z na humo ndani Weezy ametupia lyrics ambazo inafunguliwa kuwa kama amejibu lyrics za Jay-Z aka Hova kwenye goma lake na Kanye West la H.A.M iliyo kwenye collabo album na Kanye,Watch The Throne aliposema ''I’m like “Really, half a billi? Nigga, really?” You got baby money,Keep it real wit’ niggas, niggas ain’t got my lady money'' na Lil Wayne kujibu kwenye verse ya 3 “Talkin 'bout baby money? I got your baby money,Kidnap your bitch, get that 'how much you love your lady' money,I know you fake nigga, press your brakes nigga, I'll take you out, that's a date nigga”
LIL WAYNE FT DRAKE & JADAKISS

SAKATA LA MZEE YUSSUF KUUSU SHOW YA EUROPE

MZEE YUSSUF AKA MFALME - JAHAZI MODERN TAARAB
Mzee Yussuf alikua afanye show Europe kuanzia tarehe 02/09/2011 nchini Holland,tarehe 03/09 Greece,tarehe 04/09 Germany,na kudaiwa kutotia timu na kusababisha hasara ya Euro 12,000 coz maandalizi yalikua makubwa katika nchi zote ambazo alikua afanye ziara zake,Holland ticket zote tayari zilikua zimeshauzwa na kumalizika kabisa kitu ambacho kilifanya wafadhili wake watoe tena copy za nyongeza kwakua ulikua ni usiku special wa Mwafrica na raia tofauti walikua wahudhurie show hiyo
Greece halikadhalika hadi dakika za mwisho sponsor,Bw Shamir ambae alikua akiongea nae kwa njia ya simu alimuhakikishia kuwa atawasili Greece siku ya jumamosi tare 03/09 saa 10 jioni,kitu kilichowafanya kutawanya matangazo kwa watu wote hadi dakika za mwisho wananchi walikua wameshafanya shopping za nguvu kwa ajili ya kumpokea mfalme huyo,lakini hakutokea na simu zake hapokei,na kitu cha advance ameshakula kitu kilichosabaisha vurugu kwa fans wake wenye hasira coz tayari walishalipa pesa kwa ajili ya show hiyo pia kuwapa lawama waandaaji wa show hiyo kuonekana ni matapeli,kitu ambacho kimemjengea sifa mbaya kwa Europe nzima tabia ambayo inawafanya wasanii wetu kujipotezea umaarufu na ile heshima yao