Friday, September 16, 2011

SAKATA LA MZEE YUSSUF KUUSU SHOW YA EUROPE

MZEE YUSSUF AKA MFALME - JAHAZI MODERN TAARAB
Mzee Yussuf alikua afanye show Europe kuanzia tarehe 02/09/2011 nchini Holland,tarehe 03/09 Greece,tarehe 04/09 Germany,na kudaiwa kutotia timu na kusababisha hasara ya Euro 12,000 coz maandalizi yalikua makubwa katika nchi zote ambazo alikua afanye ziara zake,Holland ticket zote tayari zilikua zimeshauzwa na kumalizika kabisa kitu ambacho kilifanya wafadhili wake watoe tena copy za nyongeza kwakua ulikua ni usiku special wa Mwafrica na raia tofauti walikua wahudhurie show hiyo
Greece halikadhalika hadi dakika za mwisho sponsor,Bw Shamir ambae alikua akiongea nae kwa njia ya simu alimuhakikishia kuwa atawasili Greece siku ya jumamosi tare 03/09 saa 10 jioni,kitu kilichowafanya kutawanya matangazo kwa watu wote hadi dakika za mwisho wananchi walikua wameshafanya shopping za nguvu kwa ajili ya kumpokea mfalme huyo,lakini hakutokea na simu zake hapokei,na kitu cha advance ameshakula kitu kilichosabaisha vurugu kwa fans wake wenye hasira coz tayari walishalipa pesa kwa ajili ya show hiyo pia kuwapa lawama waandaaji wa show hiyo kuonekana ni matapeli,kitu ambacho kimemjengea sifa mbaya kwa Europe nzima tabia ambayo inawafanya wasanii wetu kujipotezea umaarufu na ile heshima yao

No comments: