Pamoja na kuwa ni wengi tumeumizwa na msiba wa aliyekuwa kiungo wa
timu ya Simba Patrick Mafisango Mutesa, lakini ni dhahiri wachezaji wenzie wa
Simba wameumizwa zaidi hasa rafiki yake kipenzi Haruna Moshi Boban.A
Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba kwa takribani masaa 24 tangu kifo
cha Mafisango kitokee Haruna Moshi ambaye wengi wetu tunamjua kama kama nunda
na mtu mwenye aibu sana lakini kufuatia msiba huu wa Mafisango, Boban amekuwa
mtu mwenye huzuni sana kiasi cha kushindwa hata kula
Kiukweli
msiba wa mwenzetu umetumuumiza sana, lakini Haruna umemuuma zaidi kwa kuwa
Mafisango ndio alikuwa rafiki yake mkubwa kuliko wachezaji wote ndani ya Simba.
Mafisango na Boban pale Simba walikuwa kama mapacha, yaani muda wote hata
tukiwa kambini utawakuta pamoja. Kwa mfano hata tukiwa tumeenda safari kwa
ajili ya mechi mara zote wenyewe walikuwa wakilala pamoja, kiukweli walikuwa
wakipendana sana na ndioa maana haishangazi kumuona Boban kwenye hali
ile." - alikaririwa akisema Emmanuel Okwi kupitia mawasiliano ya mtandao
wa BBM.
No comments:
Post a Comment