Klabu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa taji lake la kwanza la
michuano ya klabu bingwa ya Ulaya tangu kuanzishwa kwake. Chelsea wamekuwa
mabingwa baada ya kuwafunga Bayern Munich katika mchezo wa fainali kwa mikwaju
ya penati 4-3. Kwa maana hiyo Chelsea ndio inakuwa klabu ya kwanza kutoka
katika jiji la London kubeba kombe la UEFA Champions league.
Baada ya kutumia zaidi ya paundi billioni moja kwa matumizi ya
kununua wachezaji pamoja na kuwalipa mishahara na matumizi mengine tangu
kuinunua klabu ya Chelsea - hatimaye leo mmiliki wa The Blues Roman Abramovich
ametimiza ndoto yake ya kubeba taji la ulaya.
No comments:
Post a Comment