Ni fainali ambayo inatawaliwa na hadithi ya timu zote
mbili kuwakosa wachezaji muhimu, Chelsea ikiwakosa wanne na Munich ikiwakosa
watatu.
Ni fainali inayofanyika kwenye uwanja wa nyumbani wa
timu inayoshiriki mchezo wa fainali jambo ambalo linatokea kwa mara ya kwanza
kwneye kizazi hiki .
Bayern Munich moja kwa moja wanaingia kwenye mchezo
kama timu yenye nafasi kubwa ya kushinda . Ukiangalia baadhi ya factor nyingi
za ushindi ziko upande wao. Ukiangalia wachezaji watakaowakosa ni tofauti na
wale watakaokosekana na Chelsea. Munich itawakosa Luis Gustavo, David Alaba na
Olger Badstubber.
Moja ya matatizo makubwa ya Bayern Munich ni kwenye
defense na hii ni kwa sababu tofauti na ilivyo Chelsea na timu nyingine toka
England ambazo huanza kujengwa tangu nyuma kwenye defense, Bayern Munich ni
timu ambayo imeanza kujengwa kwenye safu ya ushambuliaji ambako ndio hasa ilipo
nguvu yake kuu.
Mario Gomez akisaidiwa na kina Toni Kroos,Thomas
Mueller, Arjen Robben , Franck Ribery na Bastian Schweisteiger wote wamekuwa
msaada mkubwa kwa Bayern wakati ikiwa inashambulia na ndio maana wakati
mwingine mapungufu ya Bayern kwenye defense yanashindwa kuonekana.
Hata hivyo defense ya Bayern Munich ambayo imekuwa
kwenye wakati mgumu mara nyingi imekuwa ikisaidiwa na wachezaji watakaokosekana
leo ambao ni Alaba, Badstubber na Gustavo .
Kukosekana kwa wachezaji hawa kutailazimu Bayern
pengine kuwatumia Anatoly Tymoschuk ambaye ni midfielder mwenye uwezo wa
kucheza kama beki wa kati , Philip Lahm huenda atatumika kwenye mojawapo kati
ya pande mbili za safu ya ulinzi kwa maana ya kushoto au kulia huku Bastian
Schweinsteiger akilazimika kushuka chini kucheza kama kiungo mkabaji .
Bayern ni timu ambayo ina mabao mengi ndani yake huku Mario
Gomez akiwa katikati ya mipango yote ya ufungaji . Ukitazama takwimu za msimu
huu a ligi ya mabingwa zinaonyesha kuwa Bayern Munich ni moja ya timu tatu
zilizofunga mabao mengi tangu hatua ya makundi hadi kufika fainali .
Ukiitazama Chelsea ambayo itacheza leo ndio unapata
taswira halisi ya jinsi walivyo kwenye wakati mgumu wakicheza na Bayern. Pengo
la Ramires ni kubwa pengine kuliko mapengo ya wachezaji wote watakaokosekana
kwenye line up ya Chelsea leo. Ukitazama kazi aliyoifanya ya kupunguza threat
ya Dani Alves kwenye mchezo wa nusu fainali halafu jiulize umuhimu gani
angekuwa nao kwa kumzuia mmojawapo kati ya Arjen Robben na Franck Ribery.
Ukiachilia mbali kazi ya kukaba Ramires ametokea
kurekebisha sehemu muhimu ya mchezo wake ambayo ni ufungaji wa mabao muhimu
kama alivyofanya kwenye nusu fainali dhidi ya Barca na hata kwenye fainali ya
kombe la FA .
Branislav Ivanovic naye atakuwa pengo kubwa sana kwa
Chelsea. Ivanovic ni beki mwenye umuhimu wa aina yake kwa Chelsea hasa
ukizingatia kuwa Terry hatakuwepo na Gary Cahill na David Luiz hawana match
fitnesss . Bahati mbaya naye ni mchezaji mwingine anayeingia kwenye orodha ya
watu watakaokosekana hii leo . Ukabaji wake wenye nidhamu ya ufundi hali wa
jukumu la beki pamoja na mabao yake muhimu ambayo hufunga akipanda ni jambo
ambalo linafanya kukosekana kwake kuwe mazingira magumu kwa Chelsea .
Raul Meireles ni jina lingine ambalo Chelsea
italikosa, Meireles ni kiungo ambaye hutimiza jukumu analopangiwa na kocha na
hulifanya kwa asilimia mia moja hamsini . Work Rate yake ni kubwa, na ana uwezo
wa ziada ambao kocha yoyote huhitaji kwenye timu .
Wachezaji hawa watatu wanaifanya kazi ya Chelsea kuwa
ngumu kwa kuwa wametokea kuwa misingi muhimu ya kikosi cha Chelsea chini ya
Roberto Di Matteo ambapo timu hii imekuwa ikishinda mechi nyingi kwa kufanya
kazi na kutumia nafasi chache ambazo zinapatikana .
Moja ya mambo ambayo yataamua mchezo wa fainali kwa
Chelsea ni mfumo watakaotumia. Endapo wataamua kupaki basi kwa staili
waliyoifanya dhidi ya Barca watadhurika kwa hakika kwa kuwa Bayern Munich ni
timu ambayo haina matatizo ya kiufundi ambayo yanaonekana kuidhuru Barca .
Bayern tofauti na Barca ina mpango mbadala pale mpango wake wa msingi
unaposhindikana . Ukipaki basi Bayern wanao wachezaji ambao watawatumia
kwa kupiga mashuti ya mbali kama Schweisteiger, Kroos, Lahm na Thomas Mueller .
Ukiamua kuwaelekeza mabeki au viungo wawili dhidi kucheza kwa kumkaba mmojawapo
kati ya Robben na Ribbery Bayern watatumia shimo litakalobaki katikati ya
uwanja kukudhuru na kama Chelsea watakuwa wakiokoa kwa kuwapa Bayern Umiliki wa
mpira kwenye set pieces pia watadhurika kwa kuwa Bayern wanafunga kupitia ste
pieces kwa kuwa wanae aina ya mshambuliaji ambaye Barcelona walimkosa ambaye ni
Mario Gomez na hata Chelsea wakiridhika na kutafuta sare ili wajaribu bahati ya
kwenye penati historia inaonyesha kuwa timu za ujerumani ni hatari sana kwenye
penati kama walivyotambua Real Madrid kwenye nusu fainali.
Hata hivyo Chelsea wamekuwa wakicheza vizuri wakiwa
under pressure hasa kutokana na kuridhika kuwa under dog kwenye michezo kadhaa
msimu huu.
Rudi kwenye mechi ya Barcelona na utagundua hilo. Haya
yote hayamaanishi kuwa Chelsea hawana nafasi kwani bado wanae Didier Drogba
ambaye ni mshambuliaji wa mechi kubwa . Wanaye Fernando Torres ambaye anabaki
kuwa mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kuziona nyavu .
Itakuwa fainali ngumu na isiyoamulika kirahisi ,
dakika 90 zitaamua bingwa wa ulaya msimu .
No comments:
Post a Comment