Wednesday, September 07, 2011

CHAMELEON Vs BEBE COOL BONGE LA BEEF …!

 
JOSEPH MAYANJA - CHAMELEONE
Wasanii Bebe Cool na Jose Chameleone toka Uganda,baada ya kuwa washkaji kwa sasa ni maadui aka From friends to enemies baada ya kuzinguana tena

MOSES BIDANDI SSALI - BEBE COOL
Imefunguliwa kuwa Jose Chameleone na crew yake walimkuta Bebe Cool pande za Club Rouge na kuanza mtiti ulioishia kupeana vitasa na inasemekana kuwa chanzo ni Bebe Cool aliyekuwa anamlazimisha Chameleone kutokwenda kwenye harusi ya Bobi Wine iliyofanyika August 27,2011 kwa sababu tu yeye na Bobi wine ni mahasimu
Na inadaiwa Chameleone alishambulia Bebe Cool pande za Club Rouge, na kwa kuonesha kukerwa na jambo hilo,Bebe Cool alifunguka kwenye Facebook page yake kuwa 'siamini kama Jose Chameleone angeweza kumzingua lakini anajua kuwa anataka umaarufu kwenye kurasa za mbele za magazeti,na najua unataka kujisafisha kutokana na aibu ya kuingia dini ya kiislam na sasa unataka watu wakuzungumzie kwa kugombana na mimi na wala waislamu na Wakatoliki wa Uganda hawatakusamehe kamwe kwa kutumia dini kama showbiz. May Allah bless your troubled soul'
 
Na Chalemeone naye alijibu kupitia Facebook account yake kuwa 'Huoni aibu kwa kunikataza kwenda kwenye harusi ya Bobi Wine na kuniona adui,Bebe Cool inabidi ukue na sisi si watoto tena kama jana,ona aibu kwa wivu na mdomo wako mchafu'
  
BEBE COOL vs JOSE CHAMELEONE


No comments: