Vurugu za wamachinga na mgambo
zilizotokea juzi jijini hapa, zimedaiwa kusababishwa na mvutano baina ya
ofisi ya Meya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.Zima moto shughulini.
Madai
hayo yalitolewa jana na Meya wa Jiji, Josephat Manyerere (Chadema),
wakati akizungumza wa waandishi wa habari ambapo alidai kwamba ofisi
yake haikupewa taarifa ya operesheni ya kuondoa wamachinga katika maeneo
yasiyoruhusiwa kufanya biashara katika mtaa wa Makoroboi.
Alipofuatilia,
alibaini kuwa hata ofisi ya Mbunge wa Nyamagana, haikuwa na taarifa ya
operesheni hiyo, ambayo imesababisha watu saba kujeruhiwa na kwamba
habari zilizoenezwa kuwa Chadema walihusika na vurugu hizo kwa sababu
halmashauri
inayoongozwa na chama hicho ni ya uchochezi.Amesema kwa kuwa operesheni hiyo ni
batili, amewataka wamachinga waendelee kufanya biashara katika maeneo ya
Makoroboi, hadi suala lao litakapopelekwa kwenye Baraza la Madiwani,
ili kutafutiwa utaratibu na maeneo yasiyo na bughudha. Mvutano huo wa
kiuhusiano, umesababisha ofisi ya Mkurugenzi kutotoa ushirikiano kwa
ofisi ya Meya na kutolea mfano wa uuzwaji wa viwanja katika eneo la
Kiseke bila ofisi yake kujulishwa.
Aidha, ametoa wito kwa
wamachinga kujitahidi kupanga bidhaa zao vizuri, ili watu wapate njia ya
kupita na pia wasitumie vipaza sauti kutangaza bidhaa zao na
kuhakikisha maeneo ya biashara yanabaki safi na wafanye biashara hizo
kuanzia saa 10 jioni.
Amewaomba wenye misikiti na shule katika
mtaa wa Makoroboi waendelee kuwavumilia hadi ufumbuzi wa kudumu
utakapopatikana kutokana na kwamba kulegalega kwa uhusiano wa kikazi
kumesababisha vurugu zilizotokea juzi.Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alisema watu 49 kati ya 131
waliokamatwa juzi kwenye vurugu watafikishwa mahakamani leo baada ya
uchunguzi kukamilika.
Jamani vita haina macho, binti huyu alishambuliwa akiwa anakwenda Sokoni alikotumwa na Mama yake.
Sirro amesema hali jijini hapa ni shwari na majeruhi watatu
wameonekana kuwa na majeraha ya risasi za Shot gun na uchunguzi
unafanywa kubaini walipigwa na nani kama ni mgambo au kwenye maduka
waliyovamia.
Magari yaliyochomwa moto.
Wenje
amesema kuwa yuko tayari kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu wa Kivita (ICC) The Hague, Uholanzi katika suala la kutetea haki
za wamachinga kufanya biashara katikati ya Jiji.
Hata hivyo,
Mbunge huyo amemwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda Tume ya
kuchunguza chanzo cha mgambo kupiga watu risasi kutokana na majeruhi
wengi wa vurugu hizo kuwa na majeraha ya risasi za bunduki ambazo
hazimilikiwi na Polisi.
No comments:
Post a Comment